Frequency Asked Questions
Q1. Vipi kwa wafanyakazi wanaotoka T/Bara na kazi zao za mkataba wanarejeshewa fedha zao watakapomaliza mikataba.
A. Kwa kweli hakuna taratibu za kurudisha michango kwa wanachama waliomaliza mkataba kwa sasa kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya mwaka 2005. Aidha mfuko unaangalia uwezekano wa kuandaa Muongozo wa Un Employment Benefit.
Q2. Ikiwa mwanachama hafanyi kazi tena na michango yake ipo uko je huyo atakuwa ni mwanachama wa ZSSF jambo hachangii.
A. Ikiwa uliwahi kuwa mwanachama na umesajiliwa basi hata kama umesita kuchangia basi uwanachama wake haufi.
Q3. Ili uwe mwanachama ambae utanufaika unatakiwa uchangie muda gani.
A. Ili uwe mwanachama mnufaika unatakiwa uwe umechangia kuanzia miaka 5 na kuendelea. Hapo utaweza kupata mafao endapo itathibitika kulipwa
Q4. Je vipi naweza kuchangia mwenyewe endapo mwajiri hatoniwasilishia ichango.
A. Unaweza kujichangia mwenyewe endapo umekosa ajira na ikiwa wewe unajishughulisha na kazi zake na unapata pesa basi tunamshauri aendelee na kujichangia mwenyewe na inaruhusiwa.
Q5. Vipi naweza kujiunga na Mfuko wa Uchangiaji wa Hiyari na kumchangia mtoto.
A. Unaweza kujichangia katika MFuko wa Hiyari kwa kuwasilisha kitambulisho chako kinachotumika na chenye kuonesha umri wako. Na baada yah apo utajaza Fomu ambayo inapatikana katika Ofisi za ZSSF Zilizo karibu nawe. Na Mtoto unaweza kusajiliwa kwa kuwasilishiwa kopi ya cheti chake cha kuzaliwa na picha moja. Na Mzazi ama mlezi atajaza fomu hiyo yam toto.
Q6. Kwani ZSSF isiwakopeshe wanachama wake wakati hapo kuna fedha zao.
A. Ni kweli ZSSF kuna fedha za wanachama ambazo wanaweka kwa kila mwezi. Lakini ikumbukwe kuwa mfuko huu ni wa pencheni na sio wa akiba. Hivyo lengo la kuweka fedha hizo ni kwa wakati maalum ambapo imeelezwa kwenye sheria ya Mfuko.
Q7. Tunasikia kuwa unapolipwa fedha zako na ZSSF hupewi zote unalipwa asilimia 60% na asilimia arubaini unaekewa tunaomba tueleweshwe kwanini iwe hivi.
A. Asante kwa suala zuri ambalo limeulizwa. Kwanza tuwatoe hofu wanachama wetu ya kuwa huo uvumi hauna ukweli ni maneno ya mitaani tu. Lengo la ZSSF ni lile lile ambalo limeelezwa kwenye sheria ya Mfuko. Mwanachama atachangia sasa na atalipwa wakati wa kustaafu na hakuna kitakachobakishwa baada ya kustaafu kwake. Kitakachoendelea ni malipo ya kiinua mgongo tu hadi mwisho wa Maisha yake.
Aidha ZSSF haimkati mtu fedha zake kwa sababu wakati wa kulipwa mwanachama kulipwa fedha zote alizochangia yeye na mwajiri wake na ziada ambayo huingizwa na ZSSF na mwachama huyo huonesha kima chote alichochangia na atakacholipwa. Tunawashauri wanachama wetu wakiwa na tatizo basi wafike ofisini ili kupata uhakiki wa masuala yao.
Na hii imejitokeza wakati wa mabadiliko ya baadhi ya sheria na formula ya kukokotoa mafao
Q8. Kwanini wanaume hawapati mafao ya uzazi ilhali sote tunachangia ZSSF.
A. Wanaume wao hawalipwi mafao ya uzazi kwa sababu:
- Kwanza ZSSF inaunga mkono juhudi za Serikali kusaidia akina mama na watoto wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Tunamlipa mama ili aweze kumlea mtoto wake vyema.
- Malipo haya yapo kama pilot kwanza tunangalia misuli ya mfuko.
- Kuna changamoto nyingi kwa akina baba ni mke yupi ambae atatakiwa alipwe endapo baba atakuwa na wake Zaidi ya mmoja.
- Si nchi zote wanachama wa Social Security ambao wanawalipa fao hili wanaume.
Q9. Je wanachama wanaofariki wao huwa wanapewa nyongeza kutoka ZSSF kwa sasabu wao hawapati pencheni.
A. Wanachama wanaofariki hupata malipo kwa wategemezi wao Zaidi kuliko ya wanachama wanaostaafu.
Q10. Je endapo mtoto ameekewa fedha katika Mfuko wa Hiyari na mzee anaemuelea
akafariki hili likoje.
A. Endapo itatokea mzazi wa mtoto ama mlezi amefariki basi kama atatokezea mtu ambae ataweza kumuendelezea mtoto huyu akaunti yake basi inaruhusika na endapo haiwezekani basi inaruhusiwa alipwe fedha zake zote kwa mtoto huyo.