Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ulianzishwa chini ya Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Na. 2 ya mwaka 1998, ambayo baadaye ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria Na. 9 ya mwaka 2002, na kutungwa upya kupitia Sheria Na. 2 ya mwaka 2005.

Kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo na kuanzishwa kwa ZSSF, Zanzibar haikuwa na skimu rasmi ya hifadhi ya jamii. Aidha, hakukuwa na skimu za pensheni katika sekta binafsi au zile zilizoanzishwa na waajiri kwa ajili ya wafanyakazi wao.

Kabla ya kuanzishwa kwa ZSSF, watumishi wa umma Zanzibar walihudumiwa na kupata mafao ya pensheni chini ya Sheria ya Pensheni Na. 2 ya mwaka 1990.