Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unatoa pole kwa wawekezaji, wafanyakazi, wananchi wa Nungwi na wageni wote walioathirika na janga la moto lililotokea Jumamosi, tarehe 21 Novemba 2026, katika eneo la utalii la Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambapo takriban hoteli zipatazo sita (6) pamoja na migahawa na maduka jirani. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba hakuna kifo kilichoripotiwa, na tunalipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokozi, vyombo vya ulinzi na usalama, Serikali na wananchi kwa jumla, kwa juhudi zao za haraka katika kuudhibiti moto.
WITO KWA WADAU
ZSSF inatoa wito kwa wawekezaji wote, hasa wenye majengo ya makuti, kuimarisha mifumo ya kuzima moto na kutoa mafunzo ya dharura kwa wafanyakazi. Usalama mahali pa kazi ndio kinga ya kwanza ya maisha na ajira za wafanyakazi wetu.
Ahsanteni.

