Ndugu Mwajiri, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unakukumbusha kuwasilisha michango ya wafanyakazi wako kwa wakati pamoja na nambari zao kwa usahihi. Kutomchangia mfanyakazi uliemuajiri ni kumnyima haki yake ya Hifadhi ya Jamii na ni kosa kisheria. ZSSF inakukumbusha kutekeleza wajibu wako ili kuepuka kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.


Kumbuka, tarehe 15 ya kila mwezi ni siku ya mwisho ya uwasilishaji wa michango.