Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 44 (b) cha mwaka 2005, umeanzisha Mfuko wa uchangiaji wa Hiari unaojulikana kama Zanzibar Voluntary Social Security Scheme (ZVSSS).
Mpango huu unawalenga wafuatao:-
- Wale wote ambao hawajachangia kwenye Mfuko wowote wa Hifadhi ya Jamii kutokana na ajira zao kutotegemea kipato cha kila mwezi kama vile Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Makuli, Wajasiriamali n.k,
- Wanzanibar wanaoishi nje ya nchi (Diaspora).
- Wanachama wa ZSSF na wafanyakazi walio katika Sekta rasmi.
Masharti ya Uanachama
Mtu yoyote anaweza kujiunga na Mfuko huu kwa vigezo vifuatavyo:-
- Awe na Umri usiopungua miaka 18.
- Awe na kazi inayompatia kipato halali.
Namna ya Uchangiaji
Katika Mfuko huu, akiba ya mwanachama itawekwa katika akaunti mbili tofauti. asilimia hamsini (50) itaingizwa katika akaunti ya uzeeni na asilimia hamsini (50) itaingizwa katika akaunti ya akiba ya muda mfupi.
Akaunti ya Akiba (Muda Mrefu)
Hii ni kwa ajili ya matumizi ya mara kwa mara ya wanachama kwa mfano kukuza mtaji, kulipia sehemu ya biashara, kulipia ada ya shule n.k. Mwanachama ataruhusiwa kutoa kiasi chochote cha fedha katika akaunti ya muda mfupi baada ya fedha zilizo katika akaunti ya akiba kukaa kwa muda usiopungua miezi sita.
Akaunti ya Malipo ya Uzeeni
Hii ni kwa ajili ya siku za baadae na mwanachama hataitumia hadi atakapofikia umri wa kustaafu ama atakapopoteza uwezo wa kufanya kazi. Akaunti hii inalenga kumsaidia mwanachama kuendelea kuishi maisha mazuri hata baada ya kuishiwa nguvu za kuzalisha kipato au lutokana na matatizo ya kiafya.
Mafao Yanayotolewa kwa Wanachama ni:-
- Mafao ya Uzeeni.
- Mafau ya Ulemavu.
- Mafao ya Urithi
- . Mafao ya Elimu.
- Mafao ya Wajasiriamali.





