Maelezo ya fao
Maombi ya fao la kuumia kazini yatafanywa na mfanyakazi au mtu mwengine kwa niaba ya mfanyakazi kwa Mkurugenzi Mwendeshaji mara tu mfanyakazi ataporipoti kazi baada ya kupoa majeraha, au ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya kugundulika maradhi yatokanayo na kazi, na ndani ya siku thelathini (30) kwa mwanachama aliyefariki.
Maombi hayo yataombwa kwa kujaza fomu ya maombi ya Mafao hayo (SSF 18) yakiambatanishwa na:
a) Nakala ya kadi ya uanachama ya ZSSF.
b) Cheti cha kifo (Kwa mwanachama aliefariki)
c) Taarifa ya daktari.
d) Hati ya Polisi (PF3 au PF90).
e) Taarifa ya hesabu ya benki.
f) Karatasi ya kuhudhuria Hospitali.
g) Taarifa ya ruhusa ya kutoka Hospitali.
h) Taarifa nyengine itakuwainafaa yoyote ambayo itakuwa inafaa.
i) Taarifa ya Bodi ya Madaktari (Kwa mwanachama aliepata ulemavu uliomfanya asiweze tena kurejea kazini)
Maombi ya fao la kuumia kazini hayatazingatiwa endapo hayatawasilishwa kwa Mkurugenzi Mwendeshaji ndani ya muda ulioainishwa.


