Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji Mhe. Ali Suleiman Ameir (Mrembo) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Ndg. Nassor Shaaban Ameir kwa lengo la kushukuru Wizara zilizofanya vizuri katika utiifu wa Sheria ya ZSSF, katika Wiki ya Huduma kwa Wateja hapo ofisini Mpendae Mjini Zanzibar. 8 Oktoba 2026.
Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Ndg. Saleh Daudi Makame akimhudumia mwanachama wa ZSSF katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za ZSSF Kilimani Mnara wa Mbao Zanzibar. 7 Oktoba 2026.
Mwakilishi wa ZSSF akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la mapokezi lililopambwa kwa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026.
Wafanyakazi wa ZSSF wakihudumia wateja waliokuja kupata huduma ofisini katika Wiki ya Huduma kwa Wateja, Otoba 02 -09, 2026.