Menejimenti
Mr. Nassor Shaaban Ameir
Mkurugenzi Mwendeshaji
Nd. Nassor Shaaban Ameir ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), mwenye jukumu la kutoa uongozi wa kiutendaji, kusimamia shughuli za Mfuko, utekelezaji wa mikakati na utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii.
Wasifu
Tangu alipoanza kutekeleza majukumu yake mwaka 2021, amekuwa akiongoza Menejimenti ya Mfuko katika usimamizi wa usajili wa wanachama, ukusanyaji wa michango, shughuli za uwekezaji na ulipaji wa mafao ya hifadhi ya jamii. Majukumu yake yanajumuisha kuimarisha utendaji wa taasisi, usimamizi madhubuti wa fedha na kuhakikisha huduma bora zinawafikia wanachama, waajiri na wanufaika.
Aidha, Nd. Ameir ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Afrika (ASSA), nafasi inayomwezesha kushiriki katika kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kuendeleza mifumo endelevu ya hifadhi ya jamii barani Afrika.
Kupitia nafasi yake ya uongozi, anaunga mkono dhamira ya ZSSF ya kuimarisha uwajibikaji, ufanisi wa kiutendaji, ubunifu na uendelevu wa huduma za hifadhi ya jamii Zanzibar.

