Serikali ya Mapinduzi Zanzibar emblem
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZanzibarUfunguo wa maisha ya baadaye
Mr. Saleh Daud Makame

Menejimenti

Mr. Saleh Daud Makame

Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala

Bw. Saleh Anasimamia na kufuatilia masuala ya rasilimali watu na huduma za kiutawala katika ZSSF.

Wasifu

Historia ya kitaaluma

Bw. Saleh Daud Makame ni mtaalamu wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 24 katika masuala ya usimamizi, uandaaji na uundaji wa sera, uratibu wa shughuli mbalimbali, uangalizi wa usimamizi wa rasilimali watu, pamoja na usimamizi na uendeshaji wa huduma za kiutawala. Ana uzoefu mpana katika kusimamia shughuli za taasisi, kuhakikisha utekelezaji wa sera na miongozo, kuratibu shughuli za kiutendaji, na kusimamia utoaji wa huduma za kiutawala kwa ufanisi

Elimu na sifa za kitaaluma

Ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Mashirika (Corporate Management) na Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara (Business Administration), aliyebobea katika masuala ya Masoko (Marketing). Aidha, amehitimu mafunzo ya kitaaluma kuhusu masuala mtambuka (Cross-cutting Issues) na utawala bora (Governance Affairs), yaliyomwongezea maarifa na ujuzi katika usimamizi wa taasisi, utekelezaji wa sera na taratibu, pamoja na kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika utendaji wa kazi.

Majukumu ya sasa

Kuhakikisha usimamizi na maendeleo ya rasilimali watu yenye ufanisi, utoaji bora wa huduma za kiutawala, kusimamia utekelezaji wa malengo ya kimkakati ya taasisi, kutimiza wajibu wa kisheria katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku na kuimarisha utendaji wa taasisi kwa ujumla.

Maeneo ya utaalamu

Uongozi wa kimkakati, Sheria za ajira na mahusiano ya kazi, uajiri, uteuzi na upangaji wa watumishi katika nafasi za kazi; mafunzo na maendeleo ya rasilimali watu, mahusiano baina ya mwajiri na wafanyakazi pamoja na utatuzi wa migogoro, usimamizi wa kumbukumbu na taarifa, afya na usalama kazini pamoja na ustawi wa watumishi, na usimamizi wa jumla wa shughuli za kiutawala na uendeshaji wa ofisi

Mtazamo wa uongozi

Anatumia mtindo wa uongozi wa kimkakati, shirikishi, wenye kuzingatia maadili na unaolenga matokeo. Mtindo huu wa uongozi unahimiza maendeleo ya watumishi, ufanisi wa taasisi, uwajibikaji na utekelezaji wenye mafanikio kwa malengo ya taasisi yalitowekwa.

← Rudi kwenye Menejimenti

Washirika na Wadau

Tafuta ZSSF

Fungua ukurasa wa utafutaji →

Your ZSSF Assistant

Mitandao ya kijamii
Maoni ya WatejaToa Taarifa ya UkiukwajiWhatsApp