MakaziMaduka
Iliyopo / inayotumika
Mji Wa Dr. Hussein Mwinyi
Eneo hili lipo Mombasa ambalo kwa kawaida linajulikana kama Mombasa kwa Mchina Mwanzo
Kuhusu mradi
Eneo hili lipo Mombasa ambalo kwa kawaida linajulikana kama Mombasa kwa Mchina Mwanzo, liko upande wa kulia ukiingilia kutoka barabara ya Kwa Mchina kuelekea Nyumba Mbili, pia linaweza kupatikana kupitia barabara inayojulikana kama Kwa Sheni.
Eneo hili linaunganishwa na barabara upande wake tatu (Kusini, Mashariki na Magharibi), kaskazini mwa eneo hilo kuna uzio wa makazi.
Jumla ya eneo la jengo ni m2 22,500.
Eneo lina blocks 14 ambazo kila moja itakuwa na sakafu 5 (sakafu ya chini na sakafu nyingine nne juu), ambapo idadi ya jumla ya nyumba itakuwa 276.
Kutakuwa na nyumba ya vyumba 2, 3, na 4;
• blocks 2 zitakuwa na vyumba 2
• blocks 8 zitakuwa na vyumba 3
• blocks 4 zitakuwa na vyumba 4 na maduka 30

