Mradi Mpya wa Nyumba Za Mbweni
Mradi hio upo katika eneo la Mbweni takriban kilomita moja kutoka uwanja wa ndege wa Zanzibar na kilomita 5 kutoka mji wa Zanzibar. Mahali pake maalum ni kando ya barabara ya Mbweni karibu na Chuo cha Ufundi Karume upande wa kusini.
Kuhusu mradi
Kutakuwa na vitengo vya vyumba 2, 3, na 4;
• Majengo 3 yatakuwa na vyumba 2
Majengo ya ghorofa 8 kila sakafu itakuwa na vyumba vinne hivyo jumla ya vyumba vitakuwa 96 na eneo la wastani la mita za mraba 198 kila chumba
Kila kitengo kitakuwa na chumba kimoja cha master, Chumba cha chakula, Chumba cha kukaa, Jikoni, Sehemu ya kufua nguo, Hifadhi na balcony tatu.
• Majengo 5 yatakuwa na vyumba 3
Majengo ya ghorofa 8 kila sakafu itakuwa na vyumba viwili hivyo jumla ya vyumba vitakuwa 80 na eneo la wastani la mita za mraba 357 kila chumba
Kila kitengo kitakuwa na chumba kimoja cha master, Chumba cha chakula, Chumba cha kukaa, Jikoni, Sehemu ya kufua nguo, Hifadhi na balcony tatu.
• Majengo 2 yatakuwa na vyumba 4
Majengo ya ghorofa 8 kila sakafu itakuwa na vyumba viwili hivyo jumla ya vyumba vitakuwa 32 na eneo la wastani la mita za mraba 385 kila chumba
Kila kitengo kitakuwa na vyumba viwili vya master, Chumba cha chakula, Chumba cha kukaa, Jikoni, Sehemu ya kufua nguo, Hifadhi na balcony tatu.
Kutakuwa na eneo la watoto kucheza katikati ya mtaa wa nyumba zenye vyombo vya michezo, pia kutakuwa na sehemu ya kuegesha gari katika kila jengo, bustani, taa za jua, jenereta ya dharura, usalama n.k. ambazo zitapamba eneo hilo.

