Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unaendesha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa misingi ya Shariah za Kiislamu, unaolenga kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa kuzingatia misingi ya Kiislamu. Mfuko huu unasisitiza mshikamano, uadilifu, uwazi na kusaidiana, pamoja na kuhakikisha usimamizi bora wa michango, mafao na uwekezaji kwa kuzingatia misingi ya fedha za Kiislamu (halali).
Ajali na ugojwa unaotokana na kazi ni malipo yanayolipwa kwa mwanachama wa Mfuko pale anapopata maumivu yanayotokana na ajali, maradhi yatokanayo na kazi au kifo wakati au katika kutekeleza majukumu yake ya kazi.